Mazoezi ya kazi

AMHT imejitoa hasa kushirikisha mbinu na kutoa nafasi kwa wataalamu wapya wa afya ya akili kukuza ujuzi wao katika kutoa huduma ya afya ya akili.

Mazoezi haya ya vitendo yametengenezwa kukidhi mahitaji ya mwanafunzi kwa kumalizia kozi ya shahada ya kwanza au shahada ya uzamili. Mafunzo haya yanaweza kuwa  ya wiki chache mpaka mwaka mmoja kutegemeana na  mahitaji ya mwanafunzi.

Kipaumbele cha mafunzo haya ya mazoezi kitatolewa kwa wananchi wa Tanzania.

Kwa fomu ya maombi, tafadhali tuma barua pepe pamoja na CV yako kwa info@amht.co.tz

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.