Lengo Letu

Kijiografia, Arusha Mental Health Trust inahudumia manispaa ya Arusha yenye idadi ambayo mara nyingine hudaiwa kuwa na idadi ya watu 400,000 na mara nyingine 800,000.

Lengo la AMHT ni kuhakisha utoaji wa huduma bora ya afya ya akili Arusha. Hii inafanyika hivi sasa kwa:

- Kutoa huduma ya moja kwa moja ya saikolojia na afya ya akili;
- Kupunguza unyanyapaa na kuongeza mang’amuzi juu ya afya ya akili;
- Kutoamafunzo na kuwasaidia watoaji wengine wahuduma ya afya ya akili

 

Malalamiko ya afya ya akili yameenea katika nchi hii na huduma ya afya ya akili ni ya nadra na imegubikwa na miiko mingi, haipangiwi bajeti ya kutosha na haipatikani sana kwa wale wanaohiitaji. AMHT inafanya kazi ya kutoa huduma ya akili kwa mfumo shirikishi ndani ya hospitali ya serikali, kwa kanuni ya serikali na ndani ya maelekezo ya Shirika la Afya Duniani.

Ni changamoto kwa idara ndogo ya matabibu kutekeleza mahitaji yote ya afya ya akili na kufika katika maeneo lengwa ambapo twaweza ona wateja wengi kwa bei nafuu.

 

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.