Tiba ya Afya ya Akili

Huduma ya afya ya akili inabainisha aina ya ugonjwa na kutoa tiba kwa matatizo ya akili (kama shizofrenia, sonona kali, bipolar, nk). Kutokana na kwamba hatuna daktari wa afya ya akili katika idara yetu tunawatuma wagonjwa wetu kwa madaktari wa akili sehemu nyingine kama inafaa. Kwa wale wasio na uwezo wa kuwaona madaktari wa akili, uangalizi pamoja na dawa hutolewa na wafanyakazi wetu akiwemo daktari na wauguzi wa afya ya akili waliosajiliwa. Pia tunashiriki katika utoaji wa huduma ya afya ya akili pamoja na wauuguzi wa afya ya akili wa serikali walio na chumba chao katika idara ya afya ya akili amboa huendesha klinik yao.

Saikiatri ni nini?
Madaktari wa afya ya akili ni madaktari waliobobea katika magonjwa na madawa ya afya ya akili. Madawa  siku zote yanashughukikiwa na wafanyakazi waliosomea fani hiyo na sio wanasaikolojia.

Kwa maelezo zaidi kama wataka kuweka/kupanga miadi, tafadhali bonyeza hapa

 

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.