Huduma za Kisaikolojia

Saikoloji imejikita zaidi katika taalamu zaidi ya utabibu, inaweka umuhimu katika mchakato mzima wa kufikiri, wa hisia na matendo ya watu. Kipaumbele cha Saikolojia ni kuwashauri watu juu ya afya nzuri ya akili na namna ya kuishi maisha yao.

Kwa ujumla AMHT inatoa: Tathmini ya kitabibu, kanselingi na matibabu ya kisaikolojia. Haya yote yanapatikana kutoka kwa wafanyakazi waliohitimu vema.
Wafanyakazi wa AMHT yumo tabibu wa Kisaikolojia – katika fani ya tathmini ya kitabibu na utabibu ya kisaikolojia. Jukumu lake ni kusimamia huduma za kisaikolojia zitolewazo na AMHT. Pia tunao makansela wawili. Kwa ujumla timu inafanya kazi yake kwa kufuata mfumo wa kanuni za Akili na Matendo na kuchukua mbinu zake za uponyaji.

Ni nini utabibu wa kisaikolojia, Kanseling na Tathmini?

Utabibu wa kisaikolojia unatolewa na tabibu wa saikolojia. Kwa ujumla unaitwa hivyo kwa wagonjwa ambao wanasumbuliwa sana na dalili kali za trauma, sonona ,au wasiwasi na ambao hawahitaji kuwa katika dawa. Utabibu wa kisaikolojia una mzizi wake katika fikra, hisia, muitikio wa mwili na matendo ya mtu ambayo yanachangia mkanganyiko mkubwa na kupunguza maisha mazuri ya mtu. Ni mchanganyiko kati ya mtaalamu na mteja ambao huhusisha elimu, mazungumzo ya pamoja na mabadiliko ya matendo.

Kanseling ni mchakato ambao huhusisha elimu juu ya mambo ya saikolojia, kujifunza mbinu za kukabiliana na hisia na matendo na kwa ujumla kufanya mahusiano kuwa mazuri na maisha bora. Hii hufanyika kwa makundi au kwa mtu mmoja mmoja kutokana na mahitaji ya mteja.

Tathmini ya kitabibu ni mchakato wa kugundua tatizo la afya ya akili,na kama hali hiyo yahitaji dawa au la. Pia ni mchakato uhusuo elimu, akili na matatizo ya hisia ambaya yanahitajika kushughulikiwa kwa dawa na huduma ya kisaikolojia.

Kwa maelezo zaidi kama wataka kuweka/kupanga miadi, tafadhali bonyeza hapa

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.