Karibu kwenye tovuti ya Arusha Mental Health Trust

Arusha Mental Health Trust inatoa moja kwa moja huduma ya utabibu wa afya ya kili kwa wagonjwa wa nje pia inatoa huduma ya kanselingi na utabibu wa kisaikolojia kwa watu wa makabila mbalimabli,wa jinsia zote na umri tofauti kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza.

AMHT ipo katika hosptali ya mkoa ya Mt.Meru, Arusha, Tanzania. Watu wahudumiwao kwanza ni wa eneo la Arusha  maskini na walio katika mazingira magumu kwa kupatiwa huduma ya afya ya akili na saikolojia.

Tovuti hii ni kwaajili ya kukupa maelezo juu ya masuala ya afya ya akili, huduma za afya ya akili zipatikanazo na zaidi juu ya sisi wenyewe.

Timu yetu yenye shahuku siku zote ipo tayari kusaidia na inakukaribisha katika idara yetu. Kama unalo swali lolote wasiliana nasi kwa barua pepe au kwa simu au njoo tutembelee.

Karibu sana!!

 

Saidia AMHT

Tunaelewa kuwa huduma za afya ya akili kwa nadra sana zinajilipa zenyewe hii ni kutokana na uwezo mdogo wa fedha wa watu tunaowahudumia. Hivyo, tunakuwa tegemezi kwa wafadhili kufadhili huduma zetu, ili tuweze kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali kuhudumia maskini zaidi.

Tunawashukuru wafadhili wa zamani na wasasa na tunatambua kwamba bila ya msaada wao hatutaweza kutoa huduma hizi. Tunathamini mchango wa washiriki wenza wetu na kundi la marafiki kwa ushauri wao na michango yao ya hali na mali.

.

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.