Trust
Arusha Mental Health Trust ni kampuni isiyo ya kifaida na ilisajiliwa rasmi kwa kadiri ya sheria za Tanzania tarehe 27/04/2004.
Kama Trust, Malengo ya AMHT ni:
- Kusimamia na kutoa huduma ya afya ya akili katika mji wa Arusha kwa watu wa umri wote wenye matatizo mbalimbali ya akili na kisaikolojia na wenye mahitajiya kanselingi.
- Kutoa elimu ya afya na msaada wa kisaikolojia kwa familia familia ya wateja wetu.
- Kuwa kama chemchemu ya habari kwa watu binafsi, makundi na taasisi kwa masuala yote ya afya ya akili.
- Kutafuta njia za kufundisha mbinu za msingi za kanselingi ili kuhakikisha uendelevu wa kazi ya Trust.
- Kukuza habari juu ya matunzo ya jamii kwa watu wenye matatizo ya akili kwa umma na kwa kwa mafunzo ya elimu ya kitaalamu. Hawa wana weza elezea pande zote zenye mapenzi ya afya ya akili juu ya maarifa mapya, njia na mbinu mpya za matunzo ya kijamii yanayopatikana na kuendana na mazingira halisi.
- Kutoa huduma ya makataba kwa umma ambapo vitabu viendavyo na wakati, majarida na huduma ya intaneti itapatikana.
- Kutayarisha baadhi ya maelezo na matirio ya elimu ambayo ni rahisi kusoma na yenye maelekezo mepesi kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza juu ya masuala mbalimbali ya matatizo ya afya ya akili. Vipeperuhi hivi vitahusisha pia maelezojuu ya ulevi na madawa ya kulevya.
- Kuchangia katika mafunzo, elimu na shughuli zingine ikihusisha ushirikiano katika tafiti zihusianazo na mambo ya magonjwa ya afya ya akili. Kuwa makini kwa mahitaji yeyote ya afya ya akili na kuwashirikisha wenzetu wataalamu wa tiba katika matukio ya mafunzo ya afya ya akili.
- Kutia moyo, kuelimisha watu, na kusaidia watu waelewe magonjwa ya afya ya akili eneo ambalo lina unyanyapaa mkubwa na uelewa mdogo kwa watu.
- Kuelimisha jamii na umma juu ya unyanyapaa utokanao na ulevi pamoja na madawa ya kulevya kwa waathirika na familia zao.
- Pale inapowezekana kuwa mshiriki katika uendelezaji wa kanuni/sheria za kitaifa zihusuzo kukuza mtaji wa utafiti katika kukuza uelewa wa masula ya afya ya akili na magonjwa yake.
- Kuongeza maarifa na mbinu muhimu katika kazi za afya ya akili na matunzo ya wa wagonjwa wa afya ya akili.
- Kuongeza uelewa wa watoa maamuzi, wataalamu wa afya, wafanyakazi wa elimu na kwa umma kwa ujumla juu ya ukubwa wa tatizo lihusulo magonjwa ya afya ya akili kwa watoto na vijana na namna uwezekano wa tiba yake.
- Kuongeza uelewa kwa njia rasmi na isiyo rasmi juu ya uhusiano uliopo kati ya ulemavu wa akili na umaskini.
- Kuwasaidia watu maskini wenye matatizo ya afya ya akili na familia zao kupata huduma nzuri ya afya na huduma zingine zinazohusiana na hizo.
- Kuwa kama kiungo cha mazungumzo kwa wale wenye nia ya kuanzisha au kuendeleza vituo vya kufikia, makazi ya usiku, vituo vya kuondoa sumu ya pombe na madawa ya kulevya, mawodi ya kulaza wagonjwa, madarasa au mashule ya mahitaji muhimu na vyuo vya ufundi.
Uwazi
Taasisi hii imeanzishwa maalumukwa ajili ya kuondoa umaskini au pia kwa ukuzaji wa elimu kadiri ya sehemu ya 5 ya kodi ya mapato, No: 33 ya mwaka 1973, na sehemu ya 10 ya sheria ya VAT, No: 24 ya mwaka 1997.
Bodi ya utawala ya wamiliki watatu na tustii watano hukutana kila mwaka kwa ajili ya maamuzi ya kanuni/sheri na mwelekeona pia kwa tathmini.
Changia
Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz
Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.