Sehemu yetu ya mapokezi iliyopo ndani ya uwanja wa hospitali ya serikali inafikika na kufahamika. Wakati wa wiki ya kazi wateja wanaweza kuwasiliana na wafanyakazi na kivyo kupata huduma yoyote itolewayo. Miadi kwa huduma itolewayo na wafanyakazi wa serikali pamoja na ile ya kisaikolojia inafnywa na muhudumu wamapokezi kwa umakini na upendo wa hali ya juu.
Maktaba yetu ndogo ndani ya jingo la idara ipo wazi kwa kila mtu. Tuna aina mbalimbali za vitabu, majarida na vipeperushi vya afya ya akili kwa lugha kiingereza pia huduma ya intaneti inapatikana bila ya malipo. Mambo yaliyotafsiriwa kwa Kiswahili pia hutoa elimu na habari. Maktaba yetu ndogo ni safi na yenye mazingira ya ukimya ili kumpa nafasi mwanafunzi na mteja kujisomea, kusubiria au kujipumzisha.
Maktaba ndogo na huduma ya bure ya intaneti: ni sehemu ndogo ya kuondoa unyanyapaa na kuleta watu wasio na matatizo ya afya ya akili ndani ya idara. Sisi – kupitia ufadhili wa ndani, Arusha Node Marie, tunatoa huduma ya intaneti bure kwa mtu yeyote. Ni maalumu kwa kufanyia utafiti wa kielimu na sio kwa ajili ya barua pepe kwa marafiki! Kwahiyo inafanya kazi mbili kama sehemu ya elimu na pia kwamatumaini yetu kuondoa mila potofu ya woga wa kutokuja hapa. Inaendelea kuwa huduma inayotumika vizuri. Pia tunalo darasa kubwa. Darasa hili hutumika kwa mikutano ya SIGHMA na mafunzo mengine hufanyikia humo.
Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz
Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.