Habari

Kikundi cha kusaidiana cha wazazi wa watoto wenye skizofrenia.


Tarehe 06/04/2011, tulikuwa na mkutano wa kwanza wa kikundi cha kusaidiana cha wazazi au walezi wenye mtoto mmoja au zaidi wenye skizofrenia.  Mkutano huu ulifanikiwa sana. Kikundi hiki ni jukwaa kwa familia na walezi la kupata na kupokea msaada wa kihisia na pia ni sehemu ya kubadilishana habari na uzoefu juu ya ugumu wa kumtunza mwanafamilia mwenye tatizo la skizofrenia.

Ndani ya kikundi hiki, tabibu wa afya ya akili anapatikana kuwafundisha wanafamilia juu ya ugonjwa huo na matibabu yake na kutoa msaada wa namna ya kukabiliana na tatizo kubwa la ugonjwa wa afya ya akili. Tunaamini kwamba unapotengeneza mazingira mazuri kwa mgonjwa basi mgonjwa atafaidika na familia yote itakuwa na amani/utulivu.

Mikutano inafanyika kila baada ya wiki sita katika Idara ya Afya ya Akili, hospitali ya Mt. Meru. Mkutano ujao utafanyika tarehe 18/05/2011 saa 8 mchana mpaka saa 10 jioni.

 

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.