SIGMHA (Kikundi cha walio na mapenzi ya Afya ya Akili Arusha) hukutana mara moja kwa mwezi wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana kuzungumzia masuala ya afya ya akili. AMHT akiwa mwenyeji, kikundi kipo wazi kwa wote. Kikundi hiki kimekuwa kikikutana kila mwezi na kimevutia washiriki wengi kiasi kwamba sasa tunajiuliza: tutafute sehemu nyingine ya kufanyia mikutano hii? Ijumaa wakati wa muda wa chakula cha mchana tunatoa mada maalumu za afya ya akili ili kuruhusu washiriki waweze kurudi makazini kwao baadaye. Watoa mada wawezakuwa wataalamu, wanafunzi katika vitendo, wateja, na hata wana familia walio na changamoto ya tatizo la afya ya akili.Mikutano ni wazi kwa wote. Ni sehemu muafaka ya kukutana na watu, kupata msaada binafsi, kubadilishana mawazo, kuongeza uelewa juu ya suala na pia ni sehemu ya kujijenga zaidi kitaalam kwa wafanyakazi.
Ratiba ya SIGHMA (Bonyeza Hapa)
Tunatafuta wazungumzaji. Kama una topiki yeyote ya kufurahisha, tafadhali wasiliana nasi: info@amht.co.tz
Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz
Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.