Mwanzilishi Wetu

image

Sista Sheila alizaliwa katika mji mdogo magharibi mwa Ireland mwaka 1945. Alikuwa ni mtoto wa pili wa wazazi amabao walikuwa miongoni mwa kizazi cha kwanza cha waajiriwa serikalini katika Taifa Huru jipya la Ireland. Alikulia mbali na chimbuko la babu na bibi yake wa pande zote mbili. Sheila amukuwa mgeni, mtu wa nje, mwanafunzi, mkazi, mmisionari na mtu asiye na mizizi katika nchi alizoishi ndani ya mabara matatu: Ireland, Ufaransa,Uingereza, Tanzania, Kenya, Amerika, na Ethiopia.
            Ni mkazi wa dunia na ameweza kujisikia nyumbani na kutengeneza marafiki sehemu yoyote aliyoishi. Anakubaliana na ukweli kwamba kuna wakati aliweza jisikia kama mgeni kitu ambacho anaamini ni sawa katika maisha ya umisionari. Badala ya kulichukulia jambo hili kama hasi yeye hulichukulia kama sehemu ya kujifunza ambayo kila seheme mpya hutoa. Swali lake kubwa kwa sasa kujibu ni “nyumbani ni wapi?” Anaamini sio sehemu moja, huenda ikawa ni watu,mahusiano na ile hali ya kukubalika ndio hufanya kuwa nyumbani. Ipo moyoni mwake.
            Kuishi Arusha kumempa wakati mzuri katika maisha ya Sista Sheila kwani aliwezapata marafiki wazuri, nafasi nzuri za maisha ya kiroho na nafasi ya kuweza kutoa huduma inayohitajika sana. Alijisikia kuwa ni sehemu ya jumuiya, alijulikana na alipata nafasi ya kujifunza kila siku! Anapenda miji na anafurahia kila sehemu yake, matukio, msongamano wa magari, majumba mapya na makuu, masoko, maduka, wafanya biashara wa mitaani na kuona watu wakifanya vitu mbalimbali pembezoni mwa barabara.
            Alipooulizwa juu ya zawadi, alijibu bila kusita: familia yangu, imani na marafiki. Pia alizungumzia juu ya nafasi nzuri za elimu alizopata na kwa kusita kidogo alikubaliana na ukweli kwamba alikuwa mwanafunzi bora katika shule yeyote, chuo au chuo kikuu chochote alichosomea. Sr. Sheila ………
            Alijiunga na Medical Missionaries of Mary wakati tayari akiwa kijana mwanamke  mwenye taalauma yake. Alivutiwa na shirika hili kutokana na upeowake, uchapakazi wa masista wake ambao hawakuogopeshwa na vitu vipya katika utabibu wala mazingira magumu katika tamaduni za kigeni na walifanya yote kwa upendo na tabasamu linaloambukiza.
            Amefanya kazi katika nyanja mbali mbali za utoaji wa huduma ya afya maisha yake yote ikihusisha maendeleo na mafunzo ya afya. Kazi yake ilihusisha; afya ya uzazi, mafunzo ya wakunga, huduma ya majumbani, ufundishaji rasmi na usio rasmi,  kufundisha chuo kikuu, uokozi wakati wa baa la njaa, uongozi, ushauri wa afya ya akili, mchangisha pesa, na maendeleo ya chanjo katika sehemu za jangwa kati ya jamii ya wanaohamahama. Ni mchanganyiko mkubwa wa kazi lakini siku zote alifanya akiwa na shauku pamoja na nguvu!
            Mapenzi makubwa ya Sista Sheila yalikuwa kwenye afya ya akili na alifanya juu chini kupata mafunzo mahususi na kuhamasisha juu ya matatizo mbalimabli yahusuyo afya ya akili. Kama tabibu mpya wa kisaikolojia kutoka katika chuo kikuu cha Manchester alirudi Tanzania kufanya tathmini ya mahitaji ya afya ya akili na ni huduma zipi zinahitajika. Na yaliyobaki sasa ni historia…..
            AMHT ilizaliwa barabarani na iliendelea kuishi barabarani kwa muda mrefu. Baadae ilihamia ndani ya gari lilitolewa na Malkia wa Denmak kupitia Danida, kisha ilipata makazi ya muda katika makataba ya hospitali ya Mt. Meru. Kisha baadae ilipata makazi katika chumba kidogo kimoja katika ofisi za Kanisa Katoliki na hatimaye Octoba 2000 iliweka mizizi pale ilipolichukua jingo la sasa katika hospitali ya Mkoa Mt. Meru.
            Alipoulizwa ni kitu gani kimewezesha mafanikio haya mwanzoni kabisa na kwa miaka 15 iliyopita, Sheila alikuwa wazi kwamba maneno ya mwanzilishi wa shirika lake yalilia masikioni mwake:…”Kama Mungu anaitaka kazi ataonyesha njia”. Kazi hii ilihitajika sana na kutakiwa na ilikuwa ni mikono ya Mungu kila siku. Kitu kikubwa sana alichotumiwa na Mungu ni ubia alioupata pamoja na Emmanuel Bujulu ambaye alikutana naye katika miezi ya mwanzo ya uwepo wake Arusha ambaye kwa sasa ndie Mkurugenzi mpya. Anawakumbuka watu wengi ambao walikuwa na mchango mkubwa anaogopa kuwataja kwa majina kwani anaweza sahau wengine lakini anashukuru sana kwa mchango wao mkubwa.
            Sheila alizungumzia changamoto alizokutana nazo katika huduma ya afya ya akili kama vile unyanyapaa na mila potofu juu ya ugonjwa wa afya ya akili. Pia aliongelea athari hasi za watoa huduma wengine kama vile uchawi, waganga wa jadi na waombeaji. Kwa uchungu aliongelea tatizo kubwa katika huduma ya afya ya akili ni umaskini katika hali mbalimbali.
            Huyu mwanzilishi wa kipekee sasa anajisikiaje kukabidhi kazi yake ya ukurugenzi wa AMHT? Anakubali kuwa alipata mawazo mengi na hisia mchanganyiko kama: nafuu kubwa, kushangilia, hali ya kujiona kukamilisha jambo, kujua wakati muafaka wa kuondoka na imani ya kweli kwamba kaacha nyuma yake timu yenye uwezo na kujituma. Anajisikia upweke na wasiwasi, wasiwasi wake ni juu ya upatikanaji wapesa kwa vile AMHT inategemea wafadhili kujiendesha. Anajisikia kubarikiwa kwani wakati wake wote walifanikiwa kupata wafadhili wazuri. Anashindwa kuelewa hii ilitokea namna gani zaidi ya kwamba Mungu ndiye alikuwa kiongozi katika hiyo idara. Anasema kwamba kuwa kwake sista katika Shirika lenye sifa nzuri la MMM kulisaidia, kuwa muailandi kuliongeza sifa chanya na kwa kusita anasema kuwa Sheila kuliongeza mchanganyiko wa bahati na pia usimamizi makini wa pesa ulichangia pia.
            Matumaini yake kwa AMHT ni wazi: anaomba kwamba itabakia na mtazamo wake wa huduma ya moja kwa moja kwa mteja na kipaumbele kikiwa kwa maskini na wale waishio katika mazingira magumu/hatarishi. Anapenda kuiona ikiendelea kushikilia ubora wa hali ya huu ya huduma zake, upatikanaji wake kwa watu, kubadilika kwa urahisi, uwazi na kuwa tayari kuwajibika. Anaona kuwa na mtandao, kutoa mafunzo mbalimbali, ushirika na taasisi zingine, mafunzo kwa wafanyakazi na kusoma alama za nyakati kwa njia mpya za kutoa huduma ya afya ya akili ni muhimu kwa kukinga matatizo, kutibu na kukarabati wateja. Alipooulizwa juu ya ujuzi wa timu iliyobaki, alijibu: “Inanibidi kuondoka ili kuruhusu hawa watu wazuri waweze kufanya kazi waitakayo kwa njia nzuri… ambayo kuanzia sasa ni njia yao. Ndio ninawaamini na kwa ulinzi wa Mungu wataendea katika enzi nyingine ya AMHT.
            Sheila anasubiri kwa hamu vitu vipya, sehemu mpya, changamoto mpya katika maisha yake ya huduma na majitoleo kama MMM.

 

Changia

Kujiunga na kundi la marafiki na wafadhili wetu na kupata jarida la habari kwa barua pepe, tafadhali andika kwa info@amht.co.tz

Kama wapenda kutoa mchango, tafadhali bonyeza hapa.